by Kazi Portal, 3 months ago
Ajira Portal ni mfumo mahsusi kwa ajili ya watafuta kazi wanaotaka kuomba nafasi mbalimbali ndani ya Serikalini na Utumishi wa Umma. Ajira Portal ni mfumo ambao uinasimamiwa na Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS), na inarahisisha mchakato wa kuomba kazi za serikali nchini Tanzania, ikihakikisha mchakato unaofikika kirahisi na kwa ufanisi kwa Watanzania.
Kwa watafuta kazi, kupata kazi serikalini ni muhimu sana kuwa mnatembelea ukura rasmi wa ajira portal kupitia https://portal.ajira.go.tz/. Ikiwa tayari upo registered katik mfumo huu wanaweza kuingia na kusimamia (kufuatilia muendelezo) maombi yao ya kazi, wakati watumiaji wapya wanaweza kufungua akaunti ajira portal kwa urahisi (Ukurasa rasmi wa ku-register ajira portal huonekana kama katika picha tuliyoambatanisha hapa chini).
Jinsi ya Kuingia kwenye Ajira Portal
Ili kufurahia kikamilifu fursa za ajira serikalini, ni muhimu kuelewa jinsi mchakato wa kuingia (Login) Ajira Portal unavyofanya kazi. Hapa ni hatua za kuingia:
Jinsi ya Kuunda Akaunti Mpya kwenye Ajira Portal
Kama wewe ni mtumiaji mpya, utahitaji kufungua akaunti kabla ya kuanza kuomba kazi. Mchakato wa usajili ni rahisi:
Baada ya kusajili, utaweza kuingia na kuanza kuomba kazi.
Kumbuka: Ikiwa umesahau nywila yako, unaweza kubonyeza "Forgot your password?" ili kupata maelekezo ya jinsi ya kuirejesha.
Ajira Portal ni njia rahisi na ya haraka ya kufikia nafasi za kazi serikalini Tanzania.