Overview
Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Jeshi la Polisi Tanzania 2025: Jeshi la Polisi Tanzania limetangaza tarehe rasmi ya kuanza kwa usaili kwa vijana walioomba kujiunga na Jeshi la Polisi kupitia Mtandao wa Recruitment Portal wa Jeshi la Polisi Tanzania.
Kwa mujibu wa tangazo hilo rasmi usaili huo utafanyika kuanzia tarehe 28 Aprili 2025 saa 1:00 asubuhi hadi Mei 11, 2025 na utafanyika katika maeneo mbalimbali Tanzania na Visiwani Zanzibar.
Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Jeshi la Polisi Tanzania 2025
Maeneo Rasmi ya Usaili kwa Kulingana na Kiwango cha Elimu:
1. Wenye Shahada, Stashahada na Astashahada (Degree, Diploma & Certificate Holders)
-
Usaili wao utafanyika Dar es Salaam katika uwanja wa gwaride uliopo Kambi ya Polisi (Police Barracks), barabara ya Kilwa, nyuma ya kituo cha Polisi Kilwa Road.
2. Wenye Elimu ya Kidato cha Nne na cha Sita (Form IV & Form VI)
-
Usaili wao utafanyika kwa Makamanda wa Polisi wa Mikoa ambayo waombaji walichagua wakati wa kutuma maombi.
3. Wakazi wa Zanzibar
-
Kwa walioko Unguja: Usaili utafanyika Makao Makuu ya Polisi Zanzibar (Ziwani).
-
Kwa walioko Pemba: Usaili utafanyika Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba (Chake Chake).
Vitu Muhimu vya Kubeba Siku ya Usaili:

Kila msailiwa anatakiwa kufika katika eneo la usaili akiwa na:
-
Vyeti halisi vya taaluma (academic certificates)
-
Cheti cha kuzaliwa
-
Kitambulisho cha Taifa cha NIDA au namba ya NIDA
-
Nguo za michezo na viatu vya michezo
Tahadhari Muhimu:
-
Msailiwa yeyote atakayefika kwenye usaili baada ya tarehe 28/04/2025 hatapokelewa.
-
Orodha kamili ya waliopata nafasi ya kufanya usaili imeambatishwa pamoja na tangazo hili/Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Jeshi la Polisi Tanzania 2025.
BONYEZA HAPA KUONA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA USAILI JESHI LA POLISI