Tangazo la Nafasi za Kazi – Halmashauri ya Wilaya ya Siha (10 Juni 2025)
Halmashauri ya Wilaya ya Siha inatangaza ajira kwa Watanzania wenye sifa za kujaza nafasi 9 za kazi, kufuatia kibali cha ajira kutoka Ofisi ya Rais – Utumishi wa Umma. Nafasi zilizotangazwa ni kwa ajili ya kada ya Udereva na Uhazili.
📌 Nafasi Zinazotangazwa
1. Dereva Daraja la II – Nafasi 5
Majukumu:
- Kukagua gari kabla/baada ya safari
- Kuwapeleka watumishi kwenye safari za kikazi
- Kutunza log book, kufanya usafi wa gari, kufanya matengenezo madogo
- Kusambaza nyaraka na kutekeleza maagizo ya msimamizi
Sifa:
- Kidato cha Nne, leseni Daraja E/C, uzoefu wa mwaka 1 bila ajali
- Cheti cha mafunzo ya udereva kutoka VETA au chuo kinachotambuliwa
Mshahara: Ngazi ya Serikali TGS B
2. Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II – Nafasi 4
Majukumu:
- Kuchapa barua/nyaraka, kupokea wageni, kutunza miadi na ratiba
- Kuweka kumbukumbu, kuandaa mahitaji ya ofisi, kupanga vikao
- Kusambaza majalada na taarifa ofisini
Sifa:
- Kidato cha Nne/Sita, Diploma au NTA Level 6 ya Uhazili
- Ujuzi wa hatimkato (100 maneno kwa dakika), na matumizi ya kompyuta (Word, Excel, Email, Internet)
Mshahara: Ngazi ya Serikali TGS C
📬 Maelekezo ya Maombi
- Waombaji wote wawe na umri usiozidi miaka 45
- Vyeti vya elimu na taaluma viwe vimehakikiwa na Mwanasheria
- Vyeti vya nje vihalalishwe na NECTA, TCU au NACTE
- Hakutakubaliwa: Result slips, testimonials, provisional results
- Mwisho wa kutuma maombi: 23 Juni 2025
- Tuma maombi kupitia mfumo rasmi wa ajira:
👉 https://portal.ajira.go.tz
Anuani:
Mkurugenzi Mtendaji (W),
Halmashauri ya Wilaya ya Siha,
S.L.P 129, Siha.