Tangazo la Nafasi za Kazi – Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) 10-06-2025
Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST), kupitia kibali cha ajira kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi cha tarehe 02/05/2025, kinakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi mbalimbali za kazi kwa mwaka wa fedha 2024/2025. Ajira hizi ni kwa kada mbalimbali za kitaaluma na kitaalamu katika mazingira ya elimu ya juu ya kisayansi na kiteknolojia.
Nafasi Zinazotangazwa (Jumla: 42)
Kada | Idadi ya Nafasi |
---|---|
Assistant Lecturer | 12 |
Tutorial Assistant | 8 |
Nursing Officer II | 2 |
Medical Doctor II | 1 |
Library Assistant II | 1 |
Laboratory Technician II | 7 |
Assistant Nursing Officer II | 2 |
Health Laboratory Technician II | 1 |
Laboratory Technologist II | 3 |
Planning Officer II | 1 |
Procurement and Supplies Officer II | 1 |
Assistant Supplies Officer II | 1 |
Clinical Officer II | 2 |
🧾 Sifa za Waombaji:
- Waasomi waliomaliza shahada au stashahada zinazotambulika na TCU/NACTE/NBAA/NECTA kulingana na kada husika.
- Lazima kuwa na uwezo wa kufundisha, kuchunguza, na kuchapisha tafiti kwa nafasi za Assistant Lecturer.
- Umri: Si zaidi ya miaka 45 kwa kada zote isipokuwa watumishi wa Serikali waliopo.
- Uwezo wa kutumia kompyuta kwa majukumu ya kila siku ni lazima.
📬 Maelekezo ya Maombi:
- Maombi yatumwe kwa njia ya mtandao kupitia mfumo wa ajira wa UTUMISHI:
👉 https://portal.ajira.go.tz - Mwisho wa kupokea maombi: 24 Juni 2025
- Maombi yasiyoendana na masharti au yaliyowasilishwa nje ya muda hayatafanyiwa kazi.
🏢 Anwani ya Maombi:
Makamu wa Mkuu wa Chuo,
Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya,
S.L.P. 131,
Mwanjelwa, Mbeya, Tanzania.