Tangazo la Nafasi za Kazi – Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro (10, Juni 2025)

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa kwa ajili ya kujaza nafasi tano (5) za Dereva Daraja II, kufuatia kibali kutoka Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kilichopewa tarehe 29 Aprili 2025.


📌 Nafasi ya Kazi: Dereva Daraja la II (Nafasi 5)

🛠️ Majukumu ya Kazi:

  1. Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama.
  2. Kuwapeleka watumishi maeneo ya kazi.
  3. Kufanya matengenezo madogo ya gari.
  4. Kukusanya na kusambaza nyaraka.
  5. Kutunza daftari la safari kwa usahihi.

🎓 Sifa za Mwombaji:

  • Cheti cha Kidato cha Nne.
  • Leseni ya Daraja E au C.
  • Uzoefu wa kuendesha gari kwa mwaka mmoja bila ajali.
  • Cheti cha Basic Driving Course kutoka VETA au chuo kinachotambuliwa na serikali.

💰 Mshahara:

  • Kwa mujibu wa ngazi ya Serikali: TGS B1

📌 Masharti ya Maombi:

  • Awe Mtanzania mwenye umri usiozidi miaka 45.
  • Maombi yaambatane na: barua ya maombi, CV, picha 2 ndogo, vyeti vya elimu, leseni, na vyeti vya taaluma vilivyothibitishwa.
  • “Statement of Results”, “Testmonials”, au matokeo ya kidato cha nne/sita (slips) hazitakubaliwa.
  • Vyeti vya nje vihalalishwe na NECTA, TCU au NACTE.
  • Maombi yatumiwe kupitia: https://portal.ajira.go.tz
  • Mwisho wa kutuma maombi: 22 Juni 2025
  • Anuani rasmi ya barua:
    Mkurugenzi Mtendaji,
    Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro,
    S.L.P 1880, MOROGORO

Ajira leo mabumbe, Ajira Portal, Ajira Portal News

Leave a Reply