MSANIFU MAJENGO DARAJA LA II (ARCHITECT II)(RE-ADVERTISED)
Ajira Portal
Description
APPLICATION TIMELINE: 2025-02-10 2025-02-20
Responsibilities
i.Kufanya kazi chini ya uangalizi wa Msanifu majengo aliyesajiliwa na Bodi ya Usajili husika kama “professional architect” ili kupata uzoefu unaotakiwa.
ii.Kufanya kazi kwa vitendo katika fani zinazomhusu ili kumwezesha kupata sifa za kutosha kusajiliwa na Bodi ya Usajili inayowahusu wasanifu majengo;
iii.Kufuatilia upatikanaji wa taarifa na taaluma za usanifu wa majengo;
iv.Kupitia mapendekezo ya miradi (project proposals) mbalimbali majengo yanayowasilishwa wizarani; na
v.Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na msimamizi wake wa kazi zinazoendana na sifa na fani yake
Requirements
Kuajiriwa mwenye Shahada/Stashahada ya Juu katika mojawapo ya fani zifuatazo; Architecture, Building Design, Architectural and Building Technology, Landscape Architecture, Technology in Architecture, Naval Architecture, Architectural Engineering, Furniture Architecture, Coservation Architecture, Interior Design au sifa nyingne zinazolingana na hizo ktuka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali. Awe amesajiliwa kama ‘Graduate Architect’ na Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakaridiaji Majenzi (AQRB).